Hebrews 10:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa vile sheria ni kivuli tu cha mambo mema yatakayokuja na si picha kamili ya mambo yale halisi, tambiko zilezile za sheria zinazotolewa mwaka hata mwaka, haziwezi kamwe kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Torati ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kupitia kwa dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sheria ya Musa ilitupa sisi picha tu isiyo wazi sana ya mambo yaliyokuwa yanakuja baadaye. Sheria siyo picha kamili ya mambo halisi. Sheria huwaambia watu kutoa sadaka zile zile kila mwaka. Wale wanaokuja kumwabudu Mungu wanaendelea kutoa sadaka. Lakini sheria haiwezi kamwe kuwakamilisha wao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sheria ya Wayahudi si picha kamili ya mambo yale halisi: ni kivuli tu cha mema yanayokuja. Dhabihu zilezile hutolewa daima, mwaka baada ya mwaka. Sheria yawezaje, basi, kwa njia ya dhabihu hizo, kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa vile sheria ni kivuli tu cha mambo mema yatakayokuja na si picha kamili ya mambo yale halisi, tambiko zilezile za sheria zinazotolewa mwaka hata mwaka, haziwezi kamwe kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Torati ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka, kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Torati ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wowote kuwakamilisha wakaribiao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa vile sheria ni kivuli tu cha mambo mema yatakayokuja na si picha kamili ya mambo yale halisi, tambiko zilezile za sheria zinazotolewa mwaka hata mwaka, haziwezi kamwe kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maonyo hufanana, kama ni kivuli tu cha yale mema yatakayotokea, wala siyo sura yao yenyewe, ni kufanana tu nayo. Navyo vipaji vya tambiko, walivyovipeleka kila mwaka, ni vivyo hivyo kale na kale, navyo haviwezi kuwapa utimilifu wenye kuvitoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sheria ya Kiyuda ni mufano wa mema yatakayotokea, lakini si kitambulisho kinachoonyesha mambo yale kamili. Kwa sababu hii Sheria haiwezi hata mara moja, kwa njia ya sadaka zinazotolewa mara nyingi kila mwaka, kuwafanya wakamilifu wale wanaomwendea Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.