Hebrews 10:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila kuhani Myahudi hutoa huduma yake ya ibada ya kila siku na kutoa tambiko zilezile mara nyingi, tambiko ambazo haziwezi kuondoa dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila kuhani husimama siku kwa siku akifanya huduma yake ya ibada, na kutoa tena na tena dhabihu zile zile, ambazo haziwezi kamwe kuondoa dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila siku makuhani husimama na kutekeleza shughuli zao za kidini. Tena na tena hutoa sadaka zilezile, ambazo kamwe haziwezi kuondoa dhambi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila kuhani Myahudi humhudumia Mungu kila siku, akitoa dhabibu zilezile mara nyingi, dhabibu ambazo haziwezi kuondoa dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila kuhani Myahudi hutoa huduma yake ya ibada ya kila siku na kutoa tambiko zilezile mara nyingi, tambiko ambazo haziwezi kuondoa dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila kuhani husimama siku kwa siku akifanya huduma yake ya ibada na kutoa tena na tena dhabihu zile zile ambazo haziwezi kamwe kuondoa dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila kuhani husimama siku kwa siku akifanya huduma yake ya ibada, na kutoa tena na tena dhabihu zile zile ambazo haziwezi kamwe kuondoa dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila kuhani Myahudi hutoa huduma yake ya ibada ya kila siku na kutoa tambiko zilezile mara nyingi, tambiko ambazo haziwezi kuondoa dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila mtambikaji husimama siku kwa siku akitambika, navyo vipaji vya tambiko, anavyovitoa mara nyingi, ni vivyo hivyo visivyoweza kabisa kuondoa makosa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila kuhani anasimama mbele ya Mungu kila siku kwa kufanya ibada na kutoa sadaka za namna moja mara nyingi zisizoweza hata kidogo kuondoa zambi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na killa kuhani husimama killa siku akifanya ibada, akitoa dhabihu zilezile marra nyingi; nazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.