Hebrews 10:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hili ndilo agano nitakalofanya nao, siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika akilini mwao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hili ndilo agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Mwenyezi Mungu. Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika katika nia zao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Hili ndilo agano nitakaloweka na watu wangu baadaye, asema Bwana. Nitaziweka sheria zangu ndani ya mioyo yao. Nitaziandika sheria zangu katika fahamu zao.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Hili ndilo agano nitakalofanya nao, katika siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika akilini mwao.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hili ndilo agano nitakalofanya nao, siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika akilini mwao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hili ndilo Agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Bwana. Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika katika nia zao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hili ndilo Agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Mwenyezi Mungu. Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika katika nia zao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika fikira zao nitaziandika; ndipo anenapo,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hili ndilo agano nitakalofanya nao, siku zijazo, asema Bwana: Nitaweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika akilini mwao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana anasema: Agano, nitakalolifanya nao, siku hizi zitakapokuwa zimepita, ni hili: Nitawapa maonyo yangu, yakae mioyoni mwao; tena nitayaandika katika mawazo yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Hili ndilo agano nitakalofanya nao nyuma ya siku zile. Ni Bwana wetu Mungu anayesema hivyo. Nitawawezesha kuchunga sheria zangu ndani ya mafikiri, nikiziandika ndani ya mioyo yao.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hili ni agano nitakalowapa baada ya siku zile, anna Bwana, Nitatia sharia zangu mioyoni mwao, na katika akili zao nitaziandika; ndipo anenapo.