Hebrews 10:28 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote asiyetii sheria ya Mose, huuawa bila huruma kukiwa na ushahidi wa watu wawili au watatu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeyote aliyeikataa Torati ya Musa alikufa pasipo huruma kwa ushahidi wa watu wawili au watatu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yeyote aliyekataa kuitii Sheria ya Musa alipatikana ana hatia kutokana na ushuhuda uliotolewa na mashahidi wawili au watatu. Watu wa jinsi hiyo hawakusamehewa. Waliuawa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtu yeyote asiyeitii Sheria ya Mose, huuawa bila ya huruma kukiwa na ushahidi wa watu wawili au watatu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote asiyetii sheria ya Mose, huuawa bila huruma kukiwa na ushahidi wa watu wawili au watatu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ye yote aliyeikataa sheria ya Mose alikufa pasipo huruma kwa ushahidi wa watu wawili au watatu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeyote aliyeikataa Torati ya Musa alikufa pasipo huruma kwa ushahidi wa watu wawili au watatu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu aliyeidharau Sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote asiyetii sheria ya Mose, huuawa bila huruma kukiwa na ushahidi wa watu wawili au watatu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu ayatanguaye Maonyo ya Mose huuawa pasipo kuonewa uchungu, akisutwa na mashahidi wawili au watatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote aliyevunja Sheria ya Musa, aliuawa bila huruma kisha ushuhuda wa watu wawili au watatu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu aliyeidharau sharia ya Musa, alikufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.