Hebrews 10:34 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyanganywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mliwahurumia wale waliokuwa kifungoni, mkikubali kwa furaha kunyang’anywa mali yenu kwa maana mlijua kwamba mnayo mali iliyo bora zaidi idumuyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang'anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo, mliwasaidia magerezani na kushiriki katika mateso yao. Na bado mlikuwa na furaha wakati kila kitu mlichokimiliki kilipochukuliwa kutoka kwenu. Mkaendelea kufurahi, kwa sababu mlijua kwamba mnacho kitu kilicho bora zaidi; kitu kitakachoendelea milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mlishiriki mateso ya wafungwa, na mliponyang'anywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyang'anywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mliwahurumia wale waliokuwa kifungoni, mkikubali kwa furaha kunyang'anywa mali zenu kwa maana mlijua kwamba mnayo mali iliyo bora zaidi idumuyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mliwahurumia wale waliokuwa kifungoni, mkikubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu kwa maana mlijua kwamba mnayo mali iliyo bora zaidi idumuyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang'anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyanganywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wale waliofungwa mliteseka pamoja nao; nanyi mliponyang'anywa, mliyokuwa nayo, mliitikia na kufurahi, kwani mlitambua, ya kuwa mnacho kilimbiko kiyapitacho yale kuwa kizuri, maana hakichakai.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muliwahurumia wale waliokuwa katika kifungo, nanyi mulikubali kwa furaha kunyanganywa mali zenu, kwa sababu mulijua kwamba muko na mali inayokuwa bora zaidi na yenye kudumu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo.