Hebrews 10:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwanza alisema: “Hutaki wala hupendezwi na tambiko, sadaka za kuteketezwa na za kuondoa dhambi.” Alisema hivyo ingawa sadaka hizi zote hutolewa kufuatana na sheria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwanza alisema, “Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo” (ingawa sheria iliagiza zitolewe).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati),
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwanza Kristo alisema, “Wewe hufurahishwi na sadaka na sadaka. Hukuridhishwa na sadaka za kuteketezwa na sadaka ili kuondoa dhambi.” (Hizi ndizo sadaka zote ambavyo sheria inaagiza.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwanza alisema: “Hutaki, wala hupendezwi na dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za kuondoa dhambi.” Alisema hivyo ingawa sadaka hizi zote hutolewa kufuatana na Sheria.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwanza alisema: “Hutaki wala hupendezwi na tambiko, sadaka za kuteketezwa na za kuondoa dhambi.” Alisema hivyo ingawa sadaka hizi zote hutolewa kufuatana na sheria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwanza alisema, “Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo” (ingawa sheria iliagiza zitolewe).
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwanza alisema, “Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo” (ingawa sheria iliagiza zitolewe).
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati),
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwanza alisema: “Hutaki wala hupendezwi na tambiko, sadaka za kuteketezwa na za kuondoa dhambi.” Alisema hivyo ingawa sadaka hizi zote hutolewa kufuatana na sheria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwanza anasema: Ng'ombe na vyakula vya tambiko, nazo ng'ombe za tambiko zinazoteketezwa nzima, navyo vipaji vya kulipa makosa hukuvitaka, wala hukupendezwa navyo, tena hutolewa, kama vilivyoagizwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati),
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwanza Kristo alisema: “Haukutaka wala haukupendezwa na sadaka na matoleo, wala sadaka za kuteketezwa kwa moto wala sadaka za kusamehewa zambi.” (Alisema vile ingawa sadaka hizo zote zilitolewa kufuatana na maagizo ya Sheria.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hapo juu anenapo, Dhabihu na matoleo na kafara na sadaka za dhamhi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo ilivyoamuru torati),