Hebrews 11:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Abrahamu aliamini kwamba Mungu anaweza kuwafufua wafu; na kwa namna fulani kweli Abrahamu alimpata tena mwanawe kutoka kwa wafu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ibrahimu alihesabu kuwa Mungu angeweza kumfufua Isaka kutoka kwa wafu. Na kusema kwa mfano, alimpata tena Isaka kutoka kwa wafu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aliamini kwamba Mungu angeweza kuwafufua watu kutoka kifoni. Na hakika, Mungu alipomzuia Ibrahimu katika kumuua Isaka, ilikuwa ni kama vile alimpata tena kutoka kifoni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Abrahamu aliamini kwamba Mungu anaweza kuwafufua wafu: na kwa namna fulani kweli Abrahamu alimpata tena mwanae kutoka wafu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Abrahamu aliamini kwamba Mungu anaweza kuwafufua wafu; na kwa namna fulani kweli Abrahamu alimpata tena mwanawe kutoka kwa wafu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Abrahamu alihesabu kuwa Mungu angaliweza kumfufua Isaki kutoka kwa wafu na kwa kusema kwa mfano alimpata tena Isaki kutoka kwa wafu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ibrahimu alihesabu kuwa Mungu angaliweza kumfufua Isaka kutoka kwa wafu. Na kwa kusema kwa mfano, alimpata tena Isaka kutoka kwa wafu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Abrahamu aliamini kwamba Mungu anaweza kuwafufua wafu; na kwa namna fulani kweli Abrahamu alimpata tena mwanawe kutoka kwa wafu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alidhani, ya kuwa Mungu anaweza kuamsha mtu hata kwenye wafu. Kwa hiyo alimpata tena papo hapo, alipokwisha kumtoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abrahamu aliamini kwamba Mungu anaweza kumufufua Isaka na hivi akarudishiwa tena Isaka kama vile mwenye kufufuka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.