Hebrews 11:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa imani Yakobo alipokuwa karibu kufa, aliwabariki kila mmoja wa wana wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea kichwa cha ile fimbo yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa imani Yakobo alipokuwa anakufa, alimbariki kila mmoja wa mtoto wa Yusufu, akamwabudu Mungu akiwa ameegemea juu ya kichwa cha fimbo yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa imani Yakobo, alipokuwa katika kufa, akambariki kila mmoja wa wana wa Yusufu, akaabudu akiegemea kichwa cha fimbo yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na Yakobo, pia kwa vile alikuwa na imani, alimbariki kila mmoja wa wana wa Yusufu. Alifanya haya wakati alipokuwa akifa, akaiegemea fimbo yake akimwabudu Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa imani Yakobo alipokuwa karibu kufa, aliwabariki kila mmoja wa wana wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea ile fimbo yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa imani Yakobo alipokuwa karibu kufa, aliwabariki kila mmoja wa wana wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea kichwa cha ile fimbo yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa imani Yakobo alipokuwa anakufa, alimbariki kila mmoja wa mtoto wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiwa ameegemea juu ya kichwa cha fimbo yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa imani Yakobo alipokuwa anakufa, alimbariki kila mmoja wa mtoto wa Yusufu, akamwabudu Mungu akiwa ameegemea juu ya kichwa cha fimbo yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa imani Yakobo, alipokuwa karibu kufa, akambariki kila mmoja wa wana wa Yusufu, akaabudu akiegemea kichwa cha fimbo yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa imani Yakobo alipokuwa karibu kufa, aliwabariki kila mmoja wa wana wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea kichwa cha ile fimbo yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kumtegemea Mungu Yakobo alipokuwa mwenye kufa aliwaombea mema kila mmoja wao wana wa Yosefu, akawaombea na kuinama, akiiegemea ncha ya mkongojo wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa imani Yakobo, alipokuwa katika kufa, akambariki kila mmoja wa wana wa Yusufu, akaabudu akiegemea kichwa cha fimbo yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa njia ya imani, Yakobo alipokuwa karibu kufa, alibariki kila mumoja wa wana wa Yosefu; akainama kwa kumwabudu Mungu akiegemea fimbo yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa imani Yakobo, alipokuwa katika kufa, akambariki killa mmoja wa wana wa Yusuf, akaabudu akiegemea kitanda chake.