Hebrews 11:27 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misri bila kuogopa hasira ya mfalme; na wala hakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu aliyemwona yule Mungu asiyeonekana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa imani Musa aliondoka Misri bila kuogopa ghadhabu ya mfalme. Alivumilia kwa sababu alimwona yeye asiyeonekana kwa macho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Musa akaondoka Misri kwa sababu alikuwa na imani. Hakuiogopa hasira ya mfalme. Aliendelea kuwa jasiri kama vile angemwona Mungu ambaye hakuna mtu mwingine angeweza kumwona.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misri bila kuogopa hasira ya mfalme; na wala hakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu aliyemwona yule Mungu asiyeonekana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misri bila kuogopa hasira ya mfalme; na wala hakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu aliyemwona yule Mungu asiyeonekana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa imani Mose aliondoka Misri bila kuogopa ghadhabu ya mfalme, alivumilia kwa sababu alimwona yeye asiyeonekana kwa macho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa imani Musa aliondoka Misri bila kuogopa ghadhabu ya mfalme. Alivumilia kwa sababu alimwona yeye asiyeonekana kwa macho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misri bila kuogopa hasira ya mfalme; na wala hakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu aliyemwona yule Mungu asiyeonekana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kumtegemea Mungu akatoka Misri, asiyaogope makali ya mfalme, kwani yeye asiyeonekana alishikamana naye, kama anamwona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa njia ya imani, Musa alitoka katika inchi ya Misri bila kuogopa kasirani ya mufalme. Na kama vile mutu mwenye kumwona Mungu asiyeonekana, yeye hakurudi nyuma.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa imani akatoka Misri, asiogope hasira ya mfalme; maana alistahimili kama amwonae yeye asiyeonekana.