Hebrews 11:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu; vitu vinavyoonekana kutoka vitu visivyoonekana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vyote vinavyoonekana havikuumbwa kutoka kwa vitu vinavyoonekana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Imani hutusaidia sisi kufahamu kwamba Mungu aliumba ulimwengu wote kwa amri yake. Hii inamaanisha kwamba vitu tunavyoviona viliumbwa kwa kitu kisichoonekana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu; vitu vinavyoonekana kutoka vitu visivyoonekana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu; vitu vinavyoonekana kutoka vitu visivyoonekana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vyote vinavyoonekana viliumbwa kwa vitu visivyoonekana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mwenyezi Mungu, vitu vyote vinavyoonekana havikuumbwa kutoka kwa vitu vinavyoonekana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu; vitu vinavyoonekana kutoka vitu visivyoonekana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kumtegemea Mungu twajua, ya kuwa ulimwengu ulitengenezwa kwa Neno lake Mungu, mtu asiseme: Tunavyoviona kwa macho, vilipata kuwapo kwa nguvu yao vile vinavyoonekana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa njia ya imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa amri ya Mungu, hata vitu vinavyoonekana, viliumbwa kutoka vile visivyoonekana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hatta vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.