Hebrews 11:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipigwa mawe, walipasuliwa vipandevipande, waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa watu maskini, walioteswa na kudhulumiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipigwa kwa mawe; walipasuliwa vipande viwili kwa msumeno; waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na mbuzi, wakiwa maskini, wakiteswa na kutendwa mabaya,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waliuawa kwa mawe. Walikatwa vipande viwili. Waliuawa kwa panga. Mavazi pekee wengine wao waliyokuwa nayo yalikuwa ni ngozi za kondoo au za mbuzi. Walikuwa maskini, waliteswa, na kutendewa mabaya na wengine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipigwa mawe, walipasuliwa vipandevipande, waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi, walikuwa watu maskini, walioteswa na kudhulumiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipigwa mawe, walipasuliwa vipandevipande, waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa watu maskini, walioteswa na kudhulumiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipigwa kwa mawe, walipasuliwa vipande viwili kwa msumeno, waliuawa kwa upanga, walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na mbuzi, wakiwa maskini, waliteswa na kutendwa mabaya,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipigwa kwa mawe; walipasuliwa vipande viwili kwa msumeno; waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na mbuzi, wakiwa maskini, wakiteswa na kutendwa mabaya,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizungukazunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipigwa mawe, walipasuliwa vipandevipande, waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa watu maskini, walioteswa na kudhulumiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waliuawa kwa kupigwa mawe, walipondwa, walipasuliwa, walikufa kwa kuchomwa majisu, walifukuzwa po pote, wajiendee wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi tu, wakiwa na njaa, wakiumia kwa maovu, waliyofanyiziwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wengine waliuawa kwa kutupiwa mawe, wengine walikatwa vipandevipande kwa misumeno, au kuuawa kwa upanga. Walitangatanga wakivaa ngozi za kondoo au za mbuzi, wakiishi katika umasikini, wakiteswa na kutendewa vibaya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
walipigwa mawe, walikatwa kwa msumeno, walishawishwa, waliuawa kwa upanga: walizungukazunguka, wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; waiikuwa wahitaji, wakindhiwa, wakitendwa mabaya: