Hebrews 11:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa imani Henoki alichukuliwa na Mungu, asipate kufa. Hakuonekana tena kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Maandiko yasema kwamba kabla ya kuchukuliwa kwake, yeye alikuwa amempendeza Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa imani Idrisi alitwaliwa kutoka maisha haya, kiasi kwamba hakuonja mauti. Hakuonekana, “kwa sababu Mungu alimchukua”. Kwa kuwa kabla hajatwaliwa alikuwa ameshuhudiwa kuwa ni mtu aliyempendeza Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Henoko alitwaliwa kutoka duniani, hivyo kamwe yeye hajafariki. Maandiko yanatueleza kwamba kabla ya kuchukuliwa, alikuwa mtu aliyempendeza Mungu. Baadaye, hayupo yeyote aliyejua kule alikokuwa, kwa sababu Mungu alimchukua Henoko ili awe pamoja naye. Haya yote yakatokea kwa vile alikuwa na imani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa imani Henoki alichukuliwa na Mungu, asipate kufa. Hakuonekana tena kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Maandiko yasema kwamba kabla ya kuchukuliwa kwake, yeye alikuwa amempendeza Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa imani Henoki alichukuliwa na Mungu, asipate kufa. Hakuonekana tena kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Maandiko yasema kwamba kabla ya kuchukuliwa kwake, yeye alikuwa amempendeza Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa imani Enoki alitwaliwa kutoka katika maisha haya, kiasi kwamba hakuonja mauti. Hakuonekana, kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Kwa kuwa kabla hajatwaliwa alikuwa ameshuhudiwa kuwa ni mtu aliyempendeza Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa imani Idrisi alitwaliwa kutoka maisha haya, kiasi kwamba hakuonja mauti. Hakuonekana, kwa sababu Mwenyezi Mungu alikuwa amemchukua. Kwa kuwa kabla hajatwaliwa alikuwa ameshuhudiwa kuwa ni mtu aliyempendeza Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa imani Henoki alichukuliwa na Mungu, asipate kufa. Hakuonekana tena kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Maandiko yasema kwamba kabla ya kuchukuliwa kwake, yeye alikuwa amempendeza Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kumtegemea Mungu Henoki alichukuliwa, asione kufa. Naye hakuonekana tena, kwa kuwa Mungu alikuwa amemchukua. Naye alipokuwa hajachukuliwa bado, alikuwa ameshuhudiwa, ya kuwa alimpendeza Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa njia ya imani, Enoki alibebwa na Mungu toka katika dunia pasipo kufa. Naye hakuonekana tena, kwa sababu Mungu alimubeba mbinguni. Maana Maandiko Matakatifu yanasema kwamba mbele ya kubebwa kwake, Enoki alishuhudiwa kwamba alimupendeza Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa imani Enok alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha: maana kabla ya kuhamishwa kwake alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.