Hebrews 11:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende katika nchi ambayo Mungu angempa iwe yake. Ingawa hakujua alikokuwa anakwenda, Abrahamu alihama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa imani Ibrahimu, alipoitwa aende mahali Mungu angempa baadaye kuwa urithi, alitii na akaenda, ingawa hakujua anakoenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu alimwita Ibrahimu kusafiri kwenda sehemu ingine aliyoahidi kumpa. Ibrahimu hakujua hiyo sehemu ingine ilikuwa wapi. Lakini alimtii Mungu na akaanza kusafiri kwa sababu alikuwa na imani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende katika nchi ambayo Mungu angempa iwe yake. Ingawa hakujua alikokuwa anakwenda, Abrahamu alihama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende katika nchi ambayo Mungu angempa iwe yake. Ingawa hakujua alikokuwa anakwenda, Abrahamu alihama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa imani Abrahamu, alipoitwa aende mahali ambapo Mungu angempa baadaye kuwa urithi, alitii na akaenda, ingawa hakujua anakokwenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa imani Ibrahimu, alipoitwa aende mahali ambapo Mwenyezi Mungu angempa baadaye kuwa urithi, alitii na akaenda, ingawa hakujua anakokwenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa imani Abrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende katika nchi ambayo Mungu angempa iwe yake. Ingawa hakujua alikokuwa anakwenda, Abrahamu alihama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kumtegemea Mungu Aburahamu alitii alipoitwa, ahame, aende mahali, atakapopewa kuwa urithi wake. Akahama, asijue, aendako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa njia ya imani, Abrahamu alitii wakati Mungu alipomwita na kwenda katika inchi ile Mungu aliyoahidi kumupatia kuwa urizi wake. Akaacha inchi yake pasipo kujua pahali anapokwenda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, akatoka aende hatta mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.