Hebrews 11:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi aliyoahidiwa na Mungu. Aliishi huko katika hema kama walivyoishi Isaka na Yakobo, ambao pia walishiriki ahadi ileile.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa imani alifanya maskani yake katika nchi ya ahadi kama mgeni katika nchi ya kigeni; aliishi katika mahema, kama Isaka na Yakobo walivyofanya, waliokuwa pia warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ibrahimu akaishi katika nchi ambayo Mungu aliahidi kumpa. Akaishi humo kama mgeni tu asiyekuwa mwenyeji. Alifanya hivi kwa sababu alikuwa na imani. Akaishi katika mahema pamoja na Isaka na Yakobo, ambao pia walipokea ahadi ile ile kutoka kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi aliyoahidiwa na Mungu. Aliishi huko katika hema kama walivyoishi Isaka na Yakobo, ambao pia walishiriki ahadi ileile.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi aliyoahidiwa na Mungu. Aliishi huko katika hema kama walivyoishi Isaka na Yakobo, ambao pia walishiriki ahadi ileile.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa imani alifanya maskani yake katika nchi ya ahadi kama mgeni katika nchi ya kigeni, akaishi katika mahema, kama Isaki na Yakobo walivyofanya, waliokuwa pia warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa imani alifanya maskani yake katika nchi ya ahadi kama mgeni katika nchi ya kigeni; aliishi katika mahema, kama Isaka na Yakobo walivyofanya, waliokuwa pia warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi aliyoahidiwa na Mungu. Aliishi huko katika hema kama walivyoishi Isaka na Yakobo, ambao pia walishiriki ahadi ileile.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kumtegemea Mungu akawa mgeni katika nchi, aliyoagiwa, kama siyo yake, akakaa katika mahema pamoja na Isaka na Yakobo waliokuwa wenziwe wenye urithi wa kiagio kilekile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa njia ya imani, aliishi kama vile mugeni katika inchi ile Mungu aliyomwahidi. Yeye alikuwa akiishi katika hema kama vile Isaka na Yakobo walivyoishi. Wao vilevile walishiriki pamoja naye ahadi ile ile ya Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa imani alikaa katika ile inchi ya ahadi, kama katika inchi isiyo yake, akikaa katika khema pamoja na Isaak na Yakobo, warithi pamoja nae wa ahadi ile ile.