Hebrews 12:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazazi wetu hapa duniani walituadhibu kwa muda, kama wao wenyewe walivyoona kuwa vema; lakini Mungu anatuadhibu kwa ajili ya faida yetu wenyewe, tupate kuushiriki utakatifu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baba zetu walituadibisha kwa kitambo kidogo kama wao wenyewe walivyoona vyema, lakini Mungu hutuadibisha kwa faida yetu ili tupate kushiriki utakatifu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baba zetu wa duniani waliturekebisha kwa muda mfupi katika njia waliyofikiri ilikuwa bora zaidi. Lakini Mungu huturekebisha sisi ili atusaidie tuweze kuwa watakatifu kama yeye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wazazi wetu hapa duniani walituadhibu kwa muda, kama wao wenyewe walivyoona kuwa vema; lakini Mungu anatuadhibu kwa ajili ya faida yetu wenyewe, tupate kuushiriki utakatifu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazazi wetu hapa duniani walituadhibu kwa muda, kama wao wenyewe walivyoona kuwa vema; lakini Mungu anatuadhibu kwa ajili ya faida yetu wenyewe, tupate kuushiriki utakatifu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baba zetu walituadibisha kwa kitambo kidogo kama wao wenyewe walivyoona vyema, lakini Mungu hutuadibisha kwa faida yetu ili tupate kushiriki utakatifu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baba zetu walituadibisha kwa kitambo kidogo kama wao wenyewe walivyoona vyema, lakini Mwenyezi Mungu hutuadibisha kwa faida yetu ili tupate kushiriki utakatifu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazazi wetu hapa duniani walituadhibu kwa muda, kama wao wenyewe walivyoona kuwa vema; lakini Mungu anatuadhibu kwa ajili ya faida yetu wenyewe, tupate kuushiriki utakatifu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wale waliotupiga siku chache, kama walivyowaza wenyewe kuwa vema. Lakini huyo hutupigia yafaayo, tugawiwe naye utakatifu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wababa zetu wa kimwili walituadibisha kwa siku chache kufuatana na vile walivyoona kuwa vema. Lakini Mungu anatuadibisha kwa mafaa yetu kusudi tupate kushirikiana naye katika utakatifu wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu illi tuushiriki utakatifu wake.