Hebrews 12:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuadhibiwa si jambo la kufurahisha bali la kuhuzunisha. Lakini wale waliofunzwa kuwa na nidhamu mwishowe watavuna tuzo la amani kutoka katika maisha adili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuadibishwa wakati wowote hakuonekani kuwa kitu cha kufurahisha bali chenye maumivu kinapotekelezwa. Lakini baadaye huzaa matunda ya haki na amani kwa wale waliofunzwa nayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hatufurahii marekebisho tunapokuwa tunayapata. Yanauma. Lakini baadaye, baada ya kujifunza somo kutokana na hayo, tutaifurahia amani itakayokuja kwa njia ya kufanya yaliyo sahihi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kuadhibiwa si jambo la kufurahisha bali la kuhuzunisha. Lakini wale waliofunzwa kuwa na nidhamu mwishowe watavuna tuzo la amani kutoka katika maisha adili!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuadhibiwa si jambo la kufurahisha bali la kuhuzunisha. Lakini wale waliofunzwa kuwa na nidhamu mwishowe watavuna tuzo la amani kutoka katika maisha adili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuadibishwa wakati wo wote hakuonekani kuwa kitu cha kufurahisha bali chenye maumivu kinapotekelezwa. Lakini baadaye huzaa matunda ya haki na amani kwa wale waliofunzwa nayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuadibishwa wakati wowote hakuonekani kuwa kitu cha kufurahisha bali chenye maumivu kinapotekelezwa. Lakini baadaye huzaa matunda ya haki na amani kwa wale waliofunzwa nayo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoeshwa nayo matunda ya haki yenye amani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuadhibiwa si jambo la kufurahisha bali la kuhuzunisha. Lakini wale waliofunzwa kuwa na nidhamu mwishowe watavuna tuzo la amani kutoka katika maisha adili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mapigo yote, yanapokuwapo, hatuyawazii kuwa furaha, ila masikitiko. Lakini siku za nyuma wale waliofundishwa nayo huona, yanavyowazalia matunda yenye utengemano na wongofu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maadibisho yoyote wakati yanapotolewa yanaonekana kama ni tendo la huzuni wala si la furaha. Lakini kwa mwisho yanawaletea wale waliofundishwa nayo, maisha ya amani na ya haki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Killa adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini huwatolea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.