Hebrews 12:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmefika kwa Yesu ambaye ni mpatanishi katika agano jipya, na ambaye damu yake iliyomwagika inasema mambo mema kuliko ile ya Abeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa Isa mpatanishi wa agano jipya, na kwa damu iliyonyunyizwa, ile inenayo mambo mema kuliko damu ya Habili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mmemfikia Yesu; yeye aliyelileta kutoka kwa Mungu agano jipya kwenda kwa watu wake. Mmefika kwenye damu iliyonyunyizwa ambayo inasema habari za mema zaidi kuliko damu ya Habili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mmefika kwa Yesu ambaye ameratibisha agano jipya, na ambaye damu yake iliyomwagika inasema mambo mema zaidi kuliko ile ya Abeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmefika kwa Yesu ambaye ni mpatanishi katika agano jipya, na ambaye damu yake iliyomwagika inasema mambo mema kuliko ile ya Abeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa Yesu mjumbe wa Agano Jipya na kwa damu iliyonyunyizwa, ile inenayo mambo mema kuliko damu ya Abeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa Isa mpatanishi wa agano jipya, na kwa damu iliyonyunyizwa, ile inenayo mambo mema kuliko damu ya Habili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmefika kwa Yesu ambaye ni mpatanishi katika agano jipya, na ambaye damu yake iliyomwagika inasema mambo mema kuliko ile ya Abeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, alipo naye Yesu aliyetuletea Agano Jipya, hata damu ya kunyunyizia inayosema na nguvu kuipita ile ya Abeli ipo papo hapo.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumefikia karibu na Yesu anayekuwa mupatanishi wa agano jipya, na kwenye damu yake iliyomwangwa inayosema nasi maneno mema zaidi kuliko damu ya Abeli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na Yesu mwenye kuleta agano jipya, na damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya Habil.