Hebrews 12:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi basi, na tushukuru, kwani tunapokea ufalme usiotikisika. Tuwe na shukrani na kumwabudu Mungu kwa namna itakayompendeza, kwa ibada na hofu;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, kwa kuwa tunapokea ufalme ambao hauwezi kutetemeshwa, basi na tuwe na shukrani, na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna inayompendeza, kwa unyenyekevu na uchaji,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo tunahitajika kuwa na shukrani kwa sababu tunao ufalme ambao hauwezi kutetemeshwa. Na kwa sababu sisi ni watu wa shukrani, tunahitajika kumwabudu Mungu kwa njia itakayompendeza yeye. Tunahitajika kufanya hivi kwa heshima na hofu,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sisi basi, na tushukuru kwani tunapokea utawala usiotikisika. Tuwe na shukrani na kumwabudu Mungu kwa namna itakayompendeza, kwa ibada na hofu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi basi, na tushukuru, kwani tunapokea ufalme usiotikisika. Tuwe na shukrani na kumwabudu Mungu kwa namna itakayompendeza, kwa ibada na hofu;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, kwa kuwa tunapokea ufalme ule ambao hauwezi kutetemeshwa, basi na tuwe na shukrani na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna inavyompendeza, kwa unyenyekevu na uchaji,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, kwa kuwa tunapokea ufalme ambao hauwezi kutetemeshwa, basi na tuwe na shukrani, na hivyo tumwabudu Mwenyezi Mungu kwa namna inayompendeza, kwa unyenyekevu na uchaji,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na muwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi basi, na tushukuru, kwani tunapokea ufalme usiotikisika. Tuwe na shukrani na kumwabudu Mungu kwa namna itakayompendeza, kwa ibada na hofu;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu tumepewa ufalme usiotingishika, na tuyavumishe hayo mema, tuliyogawiwa! Hivyo tutamtambikia Mungu, kama inavyompendeza, tukimcha na kumwogopa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kwa kuwa tunakubaliwa kuwa washiriki wa ufalme usioweza kutikiswa, tukuwe watu wenye shukrani. Tuonyeshe shukrani ile kwa kumwabudu Mungu kwa njia inayomupendeza kwa heshima na woga,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi tukipokea ufalme usioweza kutetemeshwa, tuwe na neema, illi kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho: