Hebrews 12:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, mmesahau yale maneno ya kutia moyo ambayo Mungu anawataja nyinyi kuwa wanawe? “Mwanangu, usidharau adhabu ya Bwana, wala usife moyo anapokukanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi mmesahau yale maneno ya kuwaonya yanayowataja ninyi kuwa wana, yakisema: “Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala usikate tamaa akikukemea,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninyi ni watoto wa Mungu, naye huzungumza maneno ya faraja kwenu. Labda mmeyasahau maneno haya: “Mwanangu, wakati Mungu anapokurekebisha, zingatia na usiache kujaribu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Je, mmesahau yale maneno ya kutia moyo ambayo Mungu anawataja ninyi kuwa wanawe? “Mwanangu, usidharau adhabu ya Bwana, wala usife moyo anapokukanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, mmesahau yale maneno ya kutia moyo ambayo Mungu anawataja nyinyi kuwa wanawe? “Mwanangu, usidharau adhabu ya Bwana, wala usife moyo anapokukanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi mmesahau yale maneno ya kuwaonya yanayowataja ninyi kuwa wana, yakisema: “Mwanangu, usidharau kuadibishwa na Bwana, wala usikate tamaa akikukemea,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi mmesahau yale maneno ya kuwaonya yanayowataja ninyi kuwa wana, yakisema: “Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala usikate tamaa akikukemea,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau maonyo ya Bwana, Wala usife moyo ukiadhibiwa naye;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, mmesahau yale maneno ya kutia moyo ambayo Mungu anawataja nyinyi kuwa wanawe? “Mwanangu, usidharau adhabu ya Bwana, wala usife moyo anapokukanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi mmeyasahau matulizo ya mioyo, aliyotuambia, ya kama tu wana wake kwamba: Mwanangu, usiseme: Si kitu, ukichapwa na Bwana, wala usilegee, unapokanywa naye!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na zaidi ya hii, mumesahau maonyo haya Mungu anayotoa kwenu kama wana wake? “Mwana wangu, usizarau azabu ya Bwana wala usiregee wakati anapokukaripia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama na wana. Mwanangu, usikudharau kurudi kwake Bwana, Wala, usizimie ukikemewa nae;