Hebrews 13:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa tambiko kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhani mkuu huchukua damu ya wanyama na kuiingiza Patakatifu pa Patakatifu, kama sadaka ya dhambi, lakini miili ya hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kuhani mkuu hubeba damu za wanyama hadi Patakatifu pa Patakatifu na hutoa damu hiyo kwa ajili ya dhambi. Lakini miili ya wanyama hao huchomwa nje ya kambi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kuhani Mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa tambiko kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhani mkuu huchukua damu ya wanyama na kuiingiza Patakatifu pa Patakatifu, kama sadaka ya dhambi, lakini miili ya hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhani mkuu huchukua damu ya wanyama na kuiingiza Patakatifu pa Patakatifu, kama sadaka ya dhambi, lakini miili ya hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa tambiko kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani damu za nyama zikiisha kupelekwa Patakatifu na mtambikaji mkuu kwa ajili ya makosa, basi, miili yao hao nyama huteketezwa nje ya kambi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani Mukubwa anapeleka damu ya nyama ndani ya Pahali Patakatifu Sana kwa ajili ya kuitoa kuwa sadaka ya kusamehewa zambi lakini viungo vyote vya nyama wale vinateketezwa kwa moto mbali na kambi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana nyama wale ambao damu yao ludetwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kituo.