Hebrews 13:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo tambiko zinazompendeza Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Na msiache kutenda mema na kushirikiana vile vitu mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na msisahau kutenda mema na kushirikishana na wengine mlivyo navyo, kwa sababu sadaka kama hizi zinamfurahisha sana Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo dhabihu zinazompendeza Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo tambiko zinazompendeza Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msiache kutenda mema na kushirikiana vile mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Na msiache kutenda mema na kushirikiana vile vitu mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo tambiko zinazompendeza Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msisahau kutenda mema na kugawiana na wenzenu yaliyo yenu! Kwani vipaji kama hivyo humpendeza Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, musisahau kutenda mema na kusaidiana, maana sadaka za namna hii zinamupendeza Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana na watu; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.