Hebrews 13:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni neno la Mungu. Fikirini juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Angalieni matokeo ya mwenendo wa maisha yao mkaiige imani yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakumbukeni viongozi wenu. Waliwafundisha ujumbe wa Mungu. Kumbukeni jinsi walivyoishi na walivyokufa, na muiige imani yao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni ujumbe wa Mungu. Fikirieni juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni neno la Mungu. Fikirini juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Angalieni matokeo ya mwenendo wa maisha yao mkaiige imani yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mwenyezi Mungu. Angalieni matokeo ya mwenendo wa maisha yao mkaiige imani yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni neno la Mungu. Fikirini juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwakumbuke waliowaongoza ninyi, waliowaambia Neno la Mungu! Tazameni, walivyotoka ulimwenguni, mviige, walivyomtegemea Mungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muwakumbuke waongozi wenu waliowatangazia neno la Mungu. Muangalie vizuri namna walivyoishi na kufa. Mufuate imani yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakumbukeni wale waliokuwa na mamlaka juu yenu, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa maisha zao, iigeni imani yao.