Hebrews 2:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ilikuwa haki tupu kwamba Mungu, ambaye huumba na kutegemeza vitu vyote, alimfanya Yesu kuwa mkamilifu kabisa kwa njia ya mateso, ili awalete watoto wengi waushiriki utukufu wake. Maana Yesu ndiye anayewaongoza kwenye wokovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ili kuwaleta wana wengi katika utukufu, ilifaa kwamba Mungu, ambaye ni kwa ajili yake na kupitia kwake kila kitu kimekuwepo, amkamilishe mwanzilishi wa wokovu wao kupitia kwa mateso yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu aliyeumba vitu vyote na ambaye kwa utukufu wake vitu vyote vipo; alitaka watu wengi wawe watoto wake na kuushiriki utukufu wake. Hivyo alifanya yale aliyohitaji kuyafanya. Alimkamilisha yeye anayewaongoza watu hao kuuelekea wokovu. Kwa njia ya mateso yake Mungu alimfanya Yesu kuwa Mwokozi mkamilifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ilikuwa haki tupu kwamba Mungu, ambaye huumba na kutegemeza vitu vyote, alimfanya Yesu kuwa mkamilifu kabisa kwa njia ya mateso, ili awalete watoto wengi waushiriki utukufu wake. Maana Yesu ndiye anayewaongoza kwenye wokovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ilikuwa haki tupu kwamba Mungu, ambaye huumba na kutegemeza vitu vyote, alimfanya Yesu kuwa mkamilifu kabisa kwa njia ya mateso, ili awalete watoto wengi waushiriki utukufu wake. Maana Yesu ndiye anayewaongoza kwenye wokovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ili kuwaleta wana wengi katika utukufu, ilimpendeza Mungu, kwa ajili yake na kwa kupitia yeye kila kitu kilichopo, kumkamilisha mwanzilishi wa wokovu wao kwa njia ya mateso.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ili kuwaleta wana wengi katika utukufu, ilifaa kwamba Mwenyezi Mungu, ambaye ni kwa ajili yake na kupitia kwake kila kitu kimekuwepo, amkamilishe mwanzilishi wa wokovu wao kwa njia ya mateso.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ilikuwa haki tupu kwamba Mungu, ambaye huumba na kutegemeza vitu vyote, alimfanya Yesu kuwa mkamilifu kabisa kwa njia ya mateso, ili awalete watoto wengi waushiriki utukufu wake. Maana Yesu ndiye anayewaongoza kwenye wokovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ni kwa ajili yake Mungu, vyote vikiwapo, naye ndiye aliyeviumba vyote; kwa hiyo ilimpasa, ile kazi ya kutimilika matesoni ampe yule aliyepeleka wana wengi kwenye utukufu alipowaokoa, apate kuwa kiongozi wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo ilifaa kwamba Mungu aliyeumba vitu vyote na kuvilinda imara, amufanye Yesu kuwa mukamilifu kwa njia ya mateso, kusudi awalete watoto wengi kuwa washiriki wa utukufu wa Mungu. Kwa maana Yesu ndiye anayewaongoza watu wapate kuokoka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa kuwa ilimpasa veye, ambae kwa ajili yake na kwa kazi yake vitu vyote vimekuwa, akileta wana wengi hatta utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokofu wao kwa mateso.