Hebrews 2:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, sisi tutaokokaje kama hatuujali wokovu mkuu kama huu? Kwanza Bwana mwenyewe aliutangaza wokovu huu, na wale waliomsikia walituthibitishia kwamba ni kweli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
je, sisi tutapataje kupona kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu, ambao mwanzo ulitangazwa na Bwana Isa, ulithibitishwa kwetu na wale waliomsikia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo kwa hakika hata nasi tutaadhibiwa kama hatutauzingatia wokovu mkuu tulionao. Alikuwa ni Bwana Yesu aliyewaambia watu kwa mara ya kwanza juu ya wokovu huo. Na wale waliomsikiliza walithibitisha kwetu kuwa yale mambo yalikuwa ni kweli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, sisi tutaokokaje kama hatuujali wokovu mkuu kama huu? Kwanza Bwana mwenyewe aliutangaza wokovu huu, na wale waliomsikia walituthibitishia kwamba ni kweli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, sisi tutaokokaje kama hatuujali wokovu mkuu kama huu? Kwanza Bwana mwenyewe aliutangaza wokovu huu, na wale waliomsikia walituthibitishia kwamba ni kweli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
je, sisi tutapaje kupona kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu, ambao mwanzo ulitangazwa na Bwana, kisha ulithibitishwa kwetu na wale waliomsikia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
je, sisi tutapaje kupona kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu, ambao mwanzo ulitangazwa na Bwana Isa, ulithibitishwa kwetu na wale waliomsikia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
sisi je! Tutapataje kupona, tukipuuza wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliomsikia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, sisi tutaokokaje kama hatuujali wokovu mkuu kama huu? Kwanza Bwana mwenyewe aliutangaza wokovu huu, na wale waliomsikia walituthibitishia kwamba ni kweli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Sisi tutalikimbia tunapoubeza wokovu ulio mkuu kama huu? Kwani ulianza kutangazwa naye Bwana, kisha ukashupazwa kwetu nao waliousikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, namna gani sisi tutaponyoka azabu kama hatushuguliki na wokovu mukubwa kama huu? Ni Bwana mwenyewe aliyetangaza kwanza habari za wokovu huu, na wale waliomusikia walihakikisha kwetu kwamba ni za kweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;