Hebrews 2:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu pia aliongeza hapo ushahidi wake kwa kufanya kila namna ya miujiza na maajabu, na kwa kuwagawia watu vipaji vya Roho Mtakatifu kadiri ya mapenzi yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia Mungu aliushuhudia kwa ishara, maajabu, na kwa miujiza mbalimbali, na karama za Roho wa Mungu alizozigawa kulingana na mapenzi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu alithibitisha hayo pia kwa kutumia ishara, maajabu, na aina zingine zote za miujiza. Na alithibitisha hayo kwa kuwapa watu vipawa tofauti kwa njia ya Roho Mtakatifu kwa namna ile aliyotaka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu pia aliongeza hapo ushahidi wake kwa kufanya kila namna ya miujiza na maajabu, na kwa kuwagawia watu vipaji vya Roho Mtakatifu kadiri ya mapenzi yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu pia aliongeza hapo ushahidi wake kwa kufanya kila namna ya miujiza na maajabu, na kwa kuwagawia watu vipaji vya Roho Mtakatifu kadiri ya mapenzi yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia Mungu aliushuhudia kwa ishara, maajabu na kwa miujiza mbalimbali, na karama za Roho Mtakatifu alizozigawa kulingana na mapenzi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia Mwenyezi Mungu aliushuhudia kwa ishara, maajabu na kwa miujiza mbalimbali, na karama za Roho wa Mwenyezi Mungu alizozigawa kulingana na mapenzi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu naye akishuhudia pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu pia aliongeza hapo ushahidi wake kwa kufanya kila namna ya miujiza na maajabu, na kwa kuwagawia watu vipaji vya Roho Mtakatifu kadiri ya mapenzi yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Mungu akaushuhudia na kufanya vielekezo na vioja na vyenye nguvu vingi na kuwagawia watu Roho takatifu kila mtu, kama alivyomtakia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu vilevile alihakikisha ushuhuda wao kwa njia ya maajabu, ya miujiza mbalimbali, na ya vitambulisho, na kwa njia ya zawadi za Roho Mutakatifu alizowapa watu kama anavyopenda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mungu nae akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.