Hebrews 2:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena yasemwa mahali fulani katika Maandiko: “Mtu ni nini, hata umfikirie; mwanadamu ni nini hata umjali?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kuna mahali mtu mmoja ameshuhudia, akisema: “Mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Imeandikwa mahali fulani katika Maandiko: “Kwa nini watu ni muhimu sana kwako? Kwa nini hata unafikiri juu yao? Kwa nini unamjali mwana wa mwanadamu? Je, yeye ni muhimu kiasi hicho?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena yasemwa mahali fulani katika Maandiko: “Mtu ni nini ee Mungu, hata umfikirie; mwanaadamu ni nini hata umjali?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena yasemwa mahali fulani katika Maandiko: “Mtu ni nini, hata umfikirie; mwanadamu ni nini hata umjali?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kuna mahali mtu fulani ameshuhudia akisema: “Mwanadamu ni kitu gani hata umfikirie, mwana wa mwanadamu ni nani hata umjali?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kuna mahali mtu fulani ameshuhudia akisema: “Mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena yasemwa mahali fulani katika Maandiko: “Mtu ni nini, hata umfikirie; mwanadamu ni nini hata umjali?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini pako paliposemwa ushuhuda wa kwamba: Mtu ndio nini, umkumbuke? Mwana wa mtu naye, umkague?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena maneno haya yanahakikishwa na pahali pengine katika Maandiko Matakatifu: “Mutu ni nini hata umukumbuke, mwanadamu ni nini hata umushugulikie?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illa mtu mmoja ameshuhudu hivi maliali fullani, Mwana Adamu ni nini hatta umkumbuke, ama mwana wa binadamu hatta umwangalie?