Hebrews 2:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ukaweka kila kitu chini ya miguu yake.” Yasemwa kwamba Mungu alimweka mtu kuwa mtawala wa vitu vyote, yaani bila kuacha hata kimoja. Hata hivyo, hatuoni bado mtu akivitawala vitu vyote sasa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nawe umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Kwa kuweka vitu vyote chini yake, Mungu hakuacha kitu chochote ambacho hakukiweka chini ya mwanadamu. Lakini kwa sasa, hatuoni kwamba kila kitu kiko chini yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ukaweka kila kitu chini ya udhibiti wake.” Kama Mungu aliweka vitu vyote chini ya udhibiti wake, basi hakikuwepo chochote kilichoachwa ambacho hakukitawala. Lakini bado hatujamwona akitawala juu ya vyote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
ukaweka kila kitu chini ya miguu yake, avitawale.” Yasemwa kwamba Mungu alimweka mtu kuwa mtawala wa vitu vyote yaani bila kuacha hata kimoja. Hata hivyo, hatuoni bado mtu akivitawala vitu vyote sasa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ukaweka kila kitu chini ya miguu yake.” Yasemwa kwamba Mungu alimweka mtu kuwa mtawala wa vitu vyote, yaani bila kuacha hata kimoja. Hata hivyo, hatuoni bado mtu akivitawala vitu vyote sasa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nawe umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Kwa kuweka vitu vyote chini yake, Mungu hakuacha kitu cho chote ambacho hakukiweka chini ya mwanadamu. Lakini kwa sasa, hatuoni kwamba kila kitu kiko chini yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nawe umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Kwa kuweka vitu vyote chini yake, Mwenyezi Mungu hakuacha kitu chochote ambacho hakukiweka chini ya mwanadamu. Lakini kwa sasa, hatuoni kwamba kila kitu kiko chini yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake. Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake hakubakiza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hamjaona vitu vyote kutiwa chini yake,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ukaweka kila kitu chini ya miguu yake.” Yasemwa kwamba Mungu alimweka mtu kuwa mtawala wa vitu vyote, yaani bila kuacha hata kimoja. Hata hivyo, hatuoni bado mtu akivitawala vitu vyote sasa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
yote pia ukayaweka kuwa chini miguuni pake. Basi, hapo, alipoviweka vyote chini yake, hakukisaza hata kimoja, asichokiweka chini yake. Lakini sasa hatujaona bado, ya kuwa vyote vimewekwa chini yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake. Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hamjaona vitu vyote kutiwa chini yake,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umemupa mamlaka juu ya vitu vyote.” Wakati inaposemwa ya kama Mungu amemupa mutu mamlaka juu ya vitu vyote, maana yake hakuacha hata kitu kimoja. Ingawa hivi, hata sasa hatuoni kwamba amepewa mamlaka juu ya vitu vyote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nmetia vitu vyote chini ya uyayo zake. Kwa maana katika kutia vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichotiwa. Illakini sasa hado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake,