Hebrews 2:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini twamwona Yesu ambaye alifanywa kwa kitambo kidogo kuwa chini kuliko malaika, ili kwa neema ya Mungu afe kwa ajili ya watu wote. Sasa tunamwona ametawazwa kwa utukufu na heshima kwa sababu ya kifo alichoteseka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini twamwona Isa, aliyefanywa chini kidogo kuliko malaika, sasa akiwa amevikwa taji la utukufu na heshima kwa sababu alistahimili mauti, ili kwa neema ya Mungu apate kuonja mauti kwa ajili ya kila mtu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa kipindi kifupi Yesu aliwekwa chini kuliko malaika, lakini sasa tunamwona akiwa amevaa taji ya utukufu na heshima kwa sababu aliteseka na kufa. Kwa sababu ya neema ya Mungu, Yesu alikufa kwa ajili ya kila mmoja.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini twamwona Yesu ambaye alifanywa kwa kitambo kidogo kuwa chini zaidi kuliko malaika, ili kwa neema ya Mungu afe kwa ajili ya watu wote. Sasa tunamwona ametawazwa kwa utukufu na heshima kwa sababu ya kifo alichoteseka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini twamwona Yesu ambaye alifanywa kwa kitambo kidogo kuwa chini kuliko malaika, ili kwa neema ya Mungu afe kwa ajili ya watu wote. Sasa tunamwona ametawazwa kwa utukufu na heshima kwa sababu ya kifo alichoteseka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini twamwona Yesu, aliyefanywa chini kidogo kuliko malaika, sasa akiwa amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu alistahimili mauti, ili kwamba kwa neema ya Mungu apate kuonja mauti kwa ajili ya kila mtu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini twamwona Isa, aliyefanywa chini kidogo kuliko malaika, sasa akiwa amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu alistahimili mauti, ili kwamba kwa neema ya Mwenyezi Mungu apate kuonja mauti kwa ajili ya kila mtu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji la utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini twamwona Yesu ambaye alifanywa kwa kitambo kidogo kuwa chini kuliko malaika, ili kwa neema ya Mungu afe kwa ajili ya watu wote. Sasa tunamwona ametawazwa kwa utukufu na heshima kwa sababu ya kifo alichoteseka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kule kwamba: Alipunguzwa kidogo, asilingane na malaika, tunaona, ya kuwa kumetimia kwake Yesu. Kwa hivyo, alivyokufa matesoni, alivikwa kilemba chenye utukufu na macheo, maana aligawiwa na Mungu, awaonjee wote uchungu wa kufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mambo tunayoona ndiyo haya: Yesu alifanywa kuwa mwenye cheo chini kidogo ya malaika kusudi kwa neema ya Mungu, Yesu akufe kwa ajili ya watu wote. Na sasa kwa njia ya kile kifo kilichomufikia, amepata utukufu na heshima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illa twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, illi kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya killa mtu.