Hebrews 3:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu zangu, watu wa Mungu ambao mmeitwa na Mungu, fikirini juu ya Yesu Mtume na Kuhani Mkuu wa imani tunayoiungama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo ndugu watakatifu, mnaoshiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini Isa, mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo, kaka na dada zangu, ninyi mliochaguliwa na Mungu muwe watu wake watakatifu, mfikirieni Yesu. Yeye ndiye tunayeamini kuwa Mungu alimtuma kuja kutuokoa na awe kuhani wetu mkuu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu zangu watu wa Mungu ambao mmeitwa na Mungu, fikirini juu ya Yesu ambaye Mungu alimtuma awe Kuhani Mkuu wa imani tunayoiungama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu zangu, watu wa Mungu ambao mmeitwa na Mungu, fikirini juu ya Yesu Mtume na Kuhani Mkuu wa imani tunayoiungama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo ndugu watakatifu, mnaoshiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini Yesu, mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo ndugu watakatifu, mnaoshiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini Isa, mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu zangu, watu wa Mungu ambao mmeitwa na Mungu, fikirini juu ya Yesu Mtume na Kuhani Mkuu wa imani tunayoiungama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo, ndugu zangu watakatifu, mlioitwa kama sisi na mwito utokao mbinguni, yaelekezeni macho kwake Yesu, tunayemwungama kuwa mtume na mtambikaji mkuu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hiyo, wandugu zangu, ninyi ambao mumeitwa na Mungu na kuwa watu wake kama vile sisi, mufikiri sana juu ya Yesu, anayekuwa mutume na Kuhani Mukubwa wa imani tunayotangaza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,