Hebrews 3:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu hiyo niliwakasirikia watu hao nikasema, ‘Fikira za watu hawa zimepotoka, hawajapata kamwe kuzijua njia zangu’.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hiyo ndiyo sababu nilikasirikia kizazi kile, nami nikasema, ‘Siku zote mioyo yao imepotoka, nao hawajazijua njia zangu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo nikawakasirikia. Nikasema, ‘Mawazo yao siku zote hayako sahihi. Hawajawahi kamwe kuzielewa njia zangu.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa sababu hiyo niliwakasirikia watu hao nikasema, Fikira za watu hawa zimepotoka, hawajapata kamwe kuzijua njia zangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu hiyo niliwakasirikia watu hao nikasema, ‘Fikira za watu hawa zimepotoka, hawajapata kamwe kuzijua njia zangu’.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hiyo ndiyo sababu nilikikasirikia kizazi kile, nami nikasema, ‘Siku zote mioyo yao hupotoka, nao hawajazijua njia zangu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hiyo ndiyo sababu nilikasirikia kizazi kile, nami nikasema, ‘Siku zote mioyo yao imepotoka, nao hawajazijua njia zangu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo nilichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu hiyo niliwakasirikia watu hao nikasema, ‘Fikira za watu hawa zimepotoka, hawajapata kamwe kuzijua njia zangu’.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikachafuliwa moyo nao wa kizazi hicho, nikasema: Siku zote hupotea njia mioyoni mwao; lakini hawakuzitambua njia zangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu ile nilikasirikia kizazi chao, na kusema: Watu hao wanapotoka siku zote. Nao hawafuati njia zangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki nikasema, Ni watu waliopotoka mioyo hawa; hawakujua njia zangu;