Hebrews 3:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mtiane moyo mtu na mwenzake kila siku, maadamu inaitwa “Leo”, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Bali mhimizane ninyi kwa ninyi kila siku, maadamu mna kitu kinachoitwa “leo.” Msaidiane ninyi kwa ninyi ili asiwepo miongoni mwenu atakayedanganywa na dhambi akawa mgumu sana kubadilika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mtiane moyo mtu na mwenzake kila siku, maadamu iitwapo Leo, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mtiane moyo mtu na mwenzake kila siku, maadamu iitwapo Leo, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mwonyane kila siku, maadamu inaitwa leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ila mwonyane wenyewe siku kwa siku, pangali pakiitwa leo, kusudi kwenu kusipatikane mwenye moyo mgumu uliodanganywa na ukosaji!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini muonyane kila siku kwa muda wote ambao lile neno “leo” linalotajwa lingali linatuelekea kusudi hata mumoja wenu asikuwe mugumu kwa kudanganywa na zambi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini muonyane killa siku, maadam iitwapo leo; mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.