Hebrews 3:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arubaini? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ni nani Mungu aliwakasirikia miaka arobaini? Je, si wale waliofanya dhambi ambao miili yao ilianguka jangwani?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na ni kina nani waliokasirikiwa na Mungu kwa miaka 40? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi. Na maiti zao zikaachwa jangwani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arobaini? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arubaini? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ni nani aliowakasirikia miaka arobaini? Je, si wale waliofanya dhambi ambao miili yao ilianguka jangwani?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ni nani aliowakasirikia miaka arobaini? Je, si wale waliofanya dhambi ambao miili yao ilianguka jangwani?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena ni akina nani waliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arubaini? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena ni akina nani waliochafua moyo wake miaka 40? Sio hao waliokosa, wao waliokufa nyikani, miili yao ikiachwa hapohapo?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, ni watu gani waliomukasirikisha Mungu kwa muda wa miaka makumi ine? Si wale wote waliofanya zambi wakaanguka na kufa katika jangwa?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na ni nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?