Hebrews 3:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu alipoapa: “Hawataingia mahali pangu pa pumziko,” alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni nani hao ambao Mungu aliapa kuwa kamwe hawataingia rahani mwake isipokuwa ni wale waliokataa kutii?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na ni watu gani ambao Mungu alikuwa akisema nao alipotoa ahadi kuwa kamwe wasingeingia mahali penye mapumziko? Alikuwa anazungumza nao ambao hawakumtii.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu alipoapa: “Hawataingia huko ambako ningewapa pumziko,” alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu alipoapa: “Hawataingia mahali pangu pa pumziko,” alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni nani hao ambao Mungu aliapa kuwa kamwe hawataingia rahani mwake isipokuwa ni wale waliokataa kutii?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni nani hao ambao Mwenyezi Mungu aliapa kuwa kamwe hawataingia rahani mwake isipokuwa ni wale waliokataa kutii?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika pumziko lake, ila wale walioasi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu alipoapa: “Hawataingia mahali pangu pa pumziko,” alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena ni akina nani, aliowaapia kwamba: Hawataingia kamwe kwenye kituo chake, wasipokuwa wale waliokataa kutii?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena ni watu gani Mungu aliowaapia kwamba hawataingia kwenye mapumziko aliyowatayarishia? Si wale waliokataa kumutii?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na ni nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, illa wale wasioamini?