Hebrews 3:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana mwenye mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Sisi wenyewe ni nyumba yake kama tukiendelea kuwa hodari na thabiti katika kile tunachotumainia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Al-Masihi ni mwaminifu kama Mwana katika nyumba ya Mungu. Sisi ndio nyumba yake, kama tutashikilia sana ujasiri wetu na tumaini tunalojivunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Kristo ni mwaminifu katika kuitawala nyumba ya Mungu kama Mwana. Nasi tu nyumba ya Mungu, kama tukibaki wajasiri katika tumaini kuu tunalofurahia kusema kuwa tunalo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana mwenye mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tukizingatia uhodari wetu na uthabiti wetu katika kile tunachotumainia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana mwenye mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Sisi wenyewe ni nyumba yake kama tukiendelea kuwa hodari na thabiti katika kile tunachotumainia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Kristo yeye ni mwaminifu kama Mwana katika nyumba ya Mungu, sisi ndio nyumba yake, kama tutashikamana sana na ujasiri wetu na katika tumaini tunalojivunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Al-Masihi ni mwaminifu kama Mwana katika nyumba ya Mwenyezi Mungu. Sisi ndio nyumba yake, kama tutashikilia sana ujasiri wetu na tumaini tunalojivunia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya tumaini letu mpaka mwisho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana mwenye mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Sisi wenyewe ni nyumba yake kama tukiendelea kuwa hodari na thabiti katika kile tunachotumainia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Kristo alitumika kama mwana aliye mwenye nyumba yake. Nayo nyumba yake ni sisi, tunapoikaza mioyo yetu, ichangamke, tena tunapofuliza kujivunia kingojeo chetu mpaka mwisho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana anayesimamia nyumba ya Mungu. Na sisi ndio nyumba ile, kama tukiendelea kuwa na uhodari na kuaminia kupata mambo tunayotumainia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho.