Hebrews 4:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, tujitahidi kuingia katika pumziko hilo, ili asiwepo yeyote miongoni mwetu atakayekataa kutii kama walivyofanya wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha hiyo, ili asiwepo yeyote atakayeanguka kwa kufuata mfano wao wa kutokutii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo hebu na tujitahidi tuwezavyo kuingia katika sehemu ya pumziko ya Mungu. Tunapaswa kujitahidi ili asiwepo miongoni mwetu atakayepotea kwa kufuata mfano wa wale waliokataa kumtii Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, tujitahidi kupata pumziko hilo, ili asiwepo yeyote miongoni mwenu atakayeshindwa, kama walivyofanya wao kwa sababu ya ukosefu wao wa imani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, tujitahidi kuingia katika pumziko hilo, ili asiwepo yeyote miongoni mwetu atakayekataa kutii kama walivyofanya wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha hiyo, ili kwamba asiwepo ye yote atakayeanguka kwa kufuata mfano wao wa kutokutii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha hiyo, ili kwamba asiwepo yeyote atakayeanguka kwa kufuata mfano wao wa kutokutii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, na tufanye bidii kuingia katika pumziko lile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano huo huo wa kuasi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, tujitahidi kuingia katika pumziko hilo, ili asiwepo yeyote miongoni mwetu atakayekataa kutii kama walivyofanya wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa tujihimize kuingia kwenye kituo kile, pasipatikane mtu atakayeangushwa akiyafuata mafunzo yao walewale waliokataa kutii!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi tufanye bidii ya kuingia kwenye mapumziko yale, kusudi hata mutu mumoja asianguke sawa vile wale walioasi katika jangwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, mtu ye yote asije akaanguka kwti mfano huo huo wa kuasi.