Hebrews 4:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, tuzingatie kwa makini imani tunayoiungama. Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka mbinguni; Yesu, Mwana wa Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu kuliko wote ambaye ameingia mbinguni, Isa Mwana wa Mungu, basi na tushikamane sana kwa uthabiti na ule ukiri wa imani yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunaye kuhani mkuu sana ambaye ameenda kuishi na Mungu kule mbinguni. Yeye ni Yesu Mwana wa Mungu. Hivyo tuendelee kuitamka imani yetu katika yeye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, tunapaswa kuzingatia kwa uthabiti imani tunayoiungama. Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka kwa Mungu mwenyewe—Yesu, Mwana wa Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, tuzingatie kwa makini imani tunayoiungama. Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka mbinguni; Yesu, Mwana wa Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu kuliko wote ambaye ameingia mbinguni, Yesu Mwana wa Mungu, basi na tushikamane sana kwa uthabiti na ule ukiri wa imani yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu kuliko wote ambaye ameingia mbinguni, Isa Mwana wa Mwenyezi Mungu, basi na tushikamane sana kwa uthabiti na ule ukiri wa imani yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, tuzingatie kwa makini imani tunayoiungama. Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka mbinguni; Yesu, Mwana wa Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tunaye mtambikaji mkuu kupita wengine aliyepaa mbinguni, ndiye Yesu, Mwana wake Mungu; kwa hiyo na tuyashike, tunayoyaungama!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, kwa kuwa tuko na Kuhani Mukubwa zaidi aliyeingia mbinguni, ndiye Yesu Mwana wa Mungu, tushikamane sana na imani tunayotangaza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, iwapo tunae kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, tujashike sana maungamo yetu.