Hebrews 4:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, hiyo ahadi ya kuingia bado ipo, maana wale waliohubiriwa Habari Njema pale awali walishindwa kuingia humo kwa sababu walikosa kutii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo inabaki kuwa wazi kwa wengine kuingia, nao wale wa kwanza waliopokea Injili walishindwa kuingia kwa sababu ya kutokutii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo fursa bado ipo kwa baadhi kuingia na kufurahia pumziko la Mungu. Lakini waliosikia kwanza habari njema juu yake hawakuweza kuingia, kwa sababu hawakutii.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale waliotangulia kuhubiriwa Habari Njema hawakupata pumziko hilo kwa sababu hawakuamini. Wapo, basi, wengine ambao wangejaliwa kulipata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, hiyo ahadi ya kuingia bado ipo, maana wale waliohubiriwa Habari Njema pale awali walishindwa kuingia humo kwa sababu walikosa kutii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo kwa kuwa inabaki kuwa wazi kwa ajili ya wengine kuingia, nao wale wa kwanza waliopokea Injili walishindwa kuingia kwa sababu ya kutokutii,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo inabaki kuwa wazi kwa wengine kuingia, nao wale wa kwanza waliopokea Injili walishindwa kuingia kwa sababu ya kutokutii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, hiyo ahadi ya kuingia bado ipo, maana wale waliohubiriwa Habari Njema pale awali walishindwa kuingia humo kwa sababu walikosa kutii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo vinajulika: wako bado watakaokiingia; lakini wale walioanza kupigiwa mbiu yake njema hawakukiingia, kwani walikataa kutii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale waliokuwa wa kwanza kuhubiriwa Habari Njema hawakuingia kwenye mapumziko yale kwa sababu ya kutokuamini kwao. Ingawa vile ingali inawezekana kwa wengine kuingia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia, na wale waliokhubiriwa khabari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,