Hebrews 4:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu aliweka siku nyingine ambayo inaitwa “Leo,” akasema baadaye kwa njia ya Daudi maneno yaliyokwisha tajwa: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiwe wakaidi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Mungu ameweka siku nyingine, akaiita “Leo”, akisema kwa kinywa cha Daudi baadaye sana, kwa maneno yaliyotangulia kunenwa: “Leo, mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu migumu”.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo Mungu akapanga siku nyingine maalumu. Inaitwa “leo.” Alizungumza juu ya siku hiyo kupitia kwa Daudi siku nyingi zilizopita kutumia maneno tuliyonukuu mwanzoni: “Kama leo mtaisikia sauti ya Mungu, msiifanye migumu mioyo yenu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Jambo hili ni wazi, kwani Mungu aliweka siku nyingine ambayo inaitwa “Leo”. Miaka mingi baadaye Mungu alisema juu ya hiyo siku kwa maneno ya Daudi katika Maandiko yaliyokwisha tajwa: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu aliweka siku nyingine ambayo inaitwa “Leo,” akasema baadaye kwa njia ya Daudi maneno yaliyokwisha tajwa: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiwe wakaidi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa hiyo Mungu ameweka siku nyingine, akaiita Leo, akisema kwa kinywa cha Daudi baadaye sana, kwa maneno yaliyotangulia kunenwa: “Leo, kama mkiisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Mwenyezi Mungu ameweka siku nyingine, akaiita Leo, akisema kwa kinywa cha Daudi baadaye sana, kwa maneno yaliyotangulia kunenwa: “Leo, kama mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu migumu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo, kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo, kama mkisikia sauti yake, Msifanye mioyo yenu migumu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu aliweka siku nyingine ambayo inaitwa “Leo,” akasema baadaye kwa njia ya Daudi maneno yaliyokwisha tajwa: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiwe wakaidi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miaka ilipokwisha kupita mingi mno, akaweka tena siku, ni hii ya leo, alipomwambia Dawidi, kama alivyosema kale: Leo, mtakapoisikia sauti yake, msiishupaze mioyo yenu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hii Mungu anaweka tena siku ingine inayoitwa “Leo”. Naye alisema juu ya siku ile nyuma ya miaka mingi kwa njia ya Daudi, kufuatana na Maandiko haya yaliyokwisha kutajwa mbele: “Leo kama munasikiliza sauti ya Mungu musifanye mioyo yenu kuwa migumu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
aweka tena siku fullani, akisema katika Daud baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo kama mtasikia sauti yake, msiifanye migumu mioyo yenu.