Hebrews 4:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama Yoshua angekuwa amewapa watu hao hilo pumziko, Mungu hangalisema baadaye juu ya siku nyingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana kama Yoshua angelikuwa amewapa raha, Mungu hangesema tena baadaye kuhusu siku nyingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunajua kuwa Yoshua hakuwaongoza watu hadi sehemu ya pumziko ambayo Mungu aliwaahidi. Tunalijua hili kwa sababu Mungu alisema baadaye kuhusu siku ya pumziko.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama Yoshua angaliwapa watu hao hilo pumziko, Mungu hangalisema baadaye juu ya siku nyingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama Yoshua angekuwa amewapa watu hao hilo pumziko, Mungu hangalisema baadaye juu ya siku nyingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana kama Yoshua alikuwa amewapa raha, Mungu hangelisema tena baadaye kuhusu siku nyingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana kama Yoshua alikuwa amewapa raha, Mwenyezi Mungu hangesema tena baadaye kuhusu siku nyingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kama Yoshua angaliwapa pumziko, asingaliinena siku nyingine baadaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama Yoshua angekuwa amewapa watu hao hilo pumziko, Mungu hangalisema baadaye juu ya siku nyingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kama Yosua angalikuwa amewapeleka kwenye kituo, asingalisema siku nyingine iliyoko nyuma bado.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana kama Yoshua angekuwa amewafikisha watu kwenye mapumziko, Mungu hangesema tena nyuma ya pale juu ya siku ingine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadae.