Hebrews 5:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila kuhani mkuu ambaye huchaguliwa miongoni mwa watu hupewa jukumu la kushughulikia mambo ya Mungu kwa niaba ya watu, kutolea zawadi na tambiko kwa ajili ya dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana kila kuhani mkuu anayechaguliwa miongoni mwa wanadamu anawekwa kuwawakilisha kwa mambo yanayomhusu Mungu, ili apate kutoa matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila kuhani Mkuu wa Kiyahudi alichaguliwa kutoka miongoni mwa watu. Kuhani huyo anapewa kazi ya kuwasaidia watu katika mambo wanayopaswa kumfanyia Mungu. Anapaswa kumtolea Mungu sadaka na sadaka za dhambi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila kuhani mkuu huchaguliwa kutoka miongoni mwa watu kwa ajili ya kumtumikia Mungu kwa niaba yao, kutolea zawadi na tambiko kwa ajili ya dhambi zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila kuhani mkuu ambaye huchaguliwa miongoni mwa watu hupewa jukumu la kushughulikia mambo ya Mungu kwa niaba ya watu, kutolea zawadi na tambiko kwa ajili ya dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana kila Kuhani Mkuu anayechaguliwa miongoni mwa wanadamu anawekwa kuwawakilisha kwa mambo yanayomhusu Mungu, ili apate kutoa matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana kila kuhani mkuu anayechaguliwa miongoni mwa wanadamu anawekwa kuwawakilisha kwa mambo yanayomhusu Mwenyezi Mungu, ili apate kutoa matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yanayomhusu Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila kuhani mkuu ambaye huchaguliwa miongoni mwa watu hupewa jukumu la kushughulikia mambo ya Mungu kwa niaba ya watu, kutolea zawadi na tambiko kwa ajili ya dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kila mtambikaji mkuu anayechaguliwa katika watu huwekwa kwa ajili ya watu, awafanyizie kazi kwake Mungu akimtolea matoleo na vipaji vya tambiko kwa ajili ya makosa yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila Kuhani Mukubwa aliyechaguliwa kati ya watu amesimikwa kwa kumutumikia Mungu kwa ajili ya watu kusudi atolee matoleo na sadaka kwa ajili ya zambi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
MAANA killa Kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wami Adamu amewekwa kwa ajili ya wana Adamu katika mambo yamkhusuyo Mungu, illi atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;