Hebrews 5:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hakuna mtu awezaye kujifanya mwenyewe kuwa kuhani mkuu. Kila mmoja huteuliwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kama alivyokuwa Aroni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakuna anayejitwalia heshima hii mwenyewe; ni lazima aitwe na Mungu, kama vile Haruni alivyoitwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kuwa kuhani mkuu ni heshima. Lakini hayupo anayejichagua mwenyewe kwa ajili ya kazi hii. Mtu huyo anapaswa kuwa amechaguliwa na Mungu kama alivyokuwa Haruni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hakuna mtu awezaye kujitwalia mwenyewe heshima ya kuwa kuhani mkuu. Kila mmoja huteuliwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kama alivyokuwa Aroni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hakuna mtu awezaye kujifanya mwenyewe kuwa kuhani mkuu. Kila mmoja huteuliwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kama alivyokuwa Aroni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakuna anayejitwalia heshima hii mwenyewe, ni lazima aitwe na Mungu, kama vile Aroni alivyoitwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakuna anayejitwalia heshima hii mwenyewe; ni lazima aitwe na Mwenyezi Mungu, kama vile Haruni alivyoitwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hakuna mtu awezaye kujifanya mwenyewe kuwa kuhani mkuu. Kila mmoja huteuliwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kama alivyokuwa Aroni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wala hakuna ajipaye mwenyewe cheo hiki, ila huitwa na Mungu, kama naye Haroni alivyoitwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakuna mutu anayejipatia heshima hii ya kuwa Kuhani Mukubwa yeye mwenyewe. Lakini anapaswa kuitwa na Mungu, kama vile Haruni alivyoitwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na hapana mtu ajitwaliae heshima hii, illa yeye aitwae na Mungu kama vile Harimi.