Hebrews 6:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu si mdhalimu: yeye hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonesha kwa ajili yake katika kuwahudumia watakatifu na hata sasa mnaendelea kuwahudumia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu ni wa haki, na ataikumbuka kila kazi mliyoifanya. Atakumbuka kuwa mliuonesha upendo wenu kwake kwa kuwasaidia watu wake na kwamba mnaendelea kuwasaidia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mlioonyesha kwa ajili ya jina lake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu si dhalimu, hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonyesha kwa ajili yake katika kuwahudumia watakatifu na kama vile mnavyoendelea kuwahudumia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwenyezi Mungu si mdhalimu: yeye hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonyesha kwa ajili yake katika kuwahudumia watakatifu na hata sasa mnaendelea kuwahudumia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Mungu siye mpotovu, hatayasahau matendo ya upendo wenu, mliyoyatumia ya kulikuza Jina lake na kuwatumikia watakatifu toka kale hata sasa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Mungu ni mwenye haki. Yeye hatasahau kazi yenu na upendo mulioonyesha kwa ajili yake kwa namna mulivyowasaidia watu wake na munavyoendelea kuwasaidia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia.