Hebrews 6:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wanapoapa, huapa kwa mmoja aliye mkuu kuliko wao, na kiapo husuluhisha ubishi wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao, nacho kiapo hicho huthibitisha kile kilichosemwa na hivyo humaliza mabishano yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mara nyingi watu hutumia jina la mtu aliye mkuu zaidi yao ili kuweka ahadi yenye kiapo. Kiapo huthibitisha kwamba walichokisema ni kweli, na hakuna haja ya kubishana juu ya hilo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wanapoapa, huapa kwa mmoja aliye mkuu zaidi kuliko wao, na kiapo hicho husuluhisha ubishi wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wanapoapa, huapa kwa mmoja aliye mkuu kuliko wao, na kiapo husuluhisha ubishi wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao, nacho kiapo hicho huthibitisha kile kilichosemwa na kumaliza mabishano yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuwaliko, nacho kiapo hicho huthibitisha kile kilichosemwa na hivyo humaliza mabishano yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao mwisho wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wanapoapa, huapa kwa mmoja aliye mkuu kuliko wao, na kiapo husuluhisha ubishi wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani watu wakiapa hutaja aliye mkubwa kuliko wao, nacho kiapo hukomesha kwao mabishano yote na kulitia nguvu lile neno.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana watu wanapofanya kiapo, wanaapa kwa jina la mutu anayekuwa mukubwa kuliko wao wenyewe, nao uhakikisho wa kiapo kile unakomesha mabishano yote kati yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana wana Adamu humwapia yeye aliye mkuu: na ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kiyathubutishe.