Hebrews 6:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kuna vitu hivi viwili: Ahadi na kiapo, ambavyo haviwezi kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyo sisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini lililowekwa mbele yetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu alifanya hivyo ili kwa vitu viwili visivyobadilika, yaani ahadi yake na kiapo chake, ambavyo kwavyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi ambao tumemkimbilia ili tulishike lile tumaini lililowekwa mbele yetu tuwe na faraja thabiti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mambo haya mawili hayawezi kubadilika: Mungu hawezi kusema uongo anaposema kitu, na hawezi kudanganya anapoweka kiapo. Hivyo mambo yote hayo ni ya msaada mkubwa kutusaidia sisi tuliomjia Mungu kwa ajili ya usalama. Yanatuhimiza kuling'ang'ania tumaini lililo letu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kuna vitu hivi viwili: ahadi na kiapo, ambavyo haviwezi kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyo sisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini lililowekwa mbele yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kuna vitu hivi viwili: ahadi na kiapo, ambavyo haviwezi kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyo sisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini lililowekwa mbele yetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu alifanya hivyo, ili kwa vitu viwili visivyobadilika, yaani ahadi yake na kiapo chake, ambavyo kwa hivyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi ambao tumemkimbilia, tuwe na moyo mkuu kulishika lile tumaini lililowekwa mbele yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwenyezi Mungu alifanya hivyo ili kwa vitu viwili visivyobadilika, yaani ahadi yake na kiapo chake, ambavyo kwavyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi ambao tumemkimbilia ili tulishike lile tumaini lililowekwa mbele yetu tuwe na faraja thabiti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kuna vitu hivi viwili: Ahadi na kiapo, ambavyo haviwezi kubadilika na wala juu ya hivyo Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hiyo sisi tuliokimbilia usalama kwake, tunapewa moyo wa kushikilia imara tumaini lililowekwa mbele yetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akataka, hayo mambo mawili yasiyotanguka kamwe - maana haiwezekani, Mungu aseme uwongo - yatupe matulizo yenye nguvu sisi tuliomkimbilia, tupate kukishika kingojeo chetu, tulichowekewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi kuna mambo mawili, ahadi na kiapo, yasiyoweza kubadilika, na kuelekea hayo, Mungu hawezi kusema uongo. Kwa hivi, sisi tuliomukimbilia tunatiwa moyo sana na kushika kwa nguvu tumaini tulilowekewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illi kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu bawezi kusema nwongo, tupate faraja lililo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;