Hebrews 6:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo lapenya mpaka mahali patakatifu mbinguni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tunalo tumaini hili kama nanga ya roho iliyo imara na thabiti. Tumaini hili huingia katika mahali patakatifu nyuma ya pazia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tumaini hili tulilonalo ni kama nanga kwetu. Ni imara na la uhakika na hutulinda salama. Huenda hadi nyuma ya pazia katika mahali patakatifu zaidi kwenye hekalu la kimbingu la Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo ni imara na thabiti, nalo lapenya lile pazia la hekalu la mbinguni mpaka patakatifu ndani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo lapenya mpaka mahali patakatifu mbinguni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tunalo tumaini hili lililo kama nanga ya roho, lililo imara na thabiti. Tumaini hili huingia katika patakatifu palipo nyuma ya pazia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tunalo tumaini hili kama nanga ya roho iliyo imara na thabiti. Tumaini hili huingia katika sehemu takatifu iliyopo nyuma ya pazia,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tunalo tumaini hilo kama nanga ya maisha yetu. Tumaini hilo lapenya mpaka mahali patakatifu mbinguni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hicho tunakishika, kiwe nanga ya moyo isiyokosa nguvu za kutuliza; nacho ndicho kituingizacho namo mle ndani, tulimopingiwa na lile pazia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tumaini hili linasimamisha imara na kulinda mioyo yetu kama vile nanga inavyosimamisha mashua imara. Nalo linapita katika pazia na kuingia katika Pahali Patakatifu Sana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo mle mlimo ndani ya pazia,