Hebrews 6:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ingawa twasema namna hii, wapenzi wetu, tuna uhakika wa kupewa mambo mema zaidi: Yaani wokovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa tunasema hivi, ndugu zangu wapendwa, kwa upande wenu tuna hakika ya mambo mema zaidi, mambo kuhusu wokovu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika habari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokovu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Rafiki zangu, sisemi haya kwa sababu nafikiri kuwa yanawatokea ninyi. Kwa hakika tunatarajia kuwa mtafanya vizuri zaidi; kwamba mtayafanya mambo mema yatakayotokea katika wokovu wenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, ingawa twasema namna hii, wapenzi wetu, tunalo tumaini kubwa juu ya hali yenu. Tunajua kwamba mmepokea baraka zile bora za wokovu wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ingawa twasema namna hii, wapenzi wetu, tuna uhakika wa kupewa mambo mema zaidi: yaani wokovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa tunasema hivi, ndugu zangu wapendwa, kwa upande wenu tuna hakika ya mambo mema zaidi, mambo yale yahusuyo wokovu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa tunasema hivi, ndugu zangu wapendwa, kwa upande wenu tuna hakika ya mambo mema zaidi, mambo yale yahusuyo wokovu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, kuhusu habari zenu tumeamini mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokovu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ingawa twasema namna hii, wapenzi wetu, tuna uhakika wa kupewa mambo mema zaidi: Yaani wokovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hata tukisema hivyo, wapendwa, kwa ajili yenu ninyi tumejipa moyo wa kwamba: Yale mema yatupayo wokovu mnayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika habari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokovu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wapendwa wangu, ijapokuwa tunasema hivi, hatuna mashaka juu yenu, tukijua kwamba munafuata njia nzuri zaidi, ile ya wokovu wenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika khabari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokofu: