Hebrews 7:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Bwana wetu ambaye mambo hayo yote yanasemwa juu yake, alikuwa wa kabila lingine, na wala hakuna hata mmoja wa kabila lake aliyepata kutumikia madhabahuni akiwa kuhani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye ambaye mambo haya yanasemwa alikuwa wa kabila lingine, na hakuna mtu wa kabila hilo aliyewahi kuhudumu katika madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kabila nyingine, ambayo hapana mtu wa kabila hiyo aliyeihudumia madhabahu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunazungumza juu ya Bwana Yesu, aliyetoka katika kabila lingine. Hakuwepo yeyote kutoka katika kabila hilo kamwe aliyeweza kutumika kama kuhani madhabahuni. Ni dhahiri kwamba Bwana Yesu alitoka katika kabila la Yuda. Na Musa hakusema chochote kuhusu makuhani waliyetokana na kabila hilo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye Bwana wetu ambaye mambo hayo yote yanasemwa juu yake, alikuwa wa kabila lingine, na wala hakuna hata mmoja wa kabila lake aliyepata kutumikia madhabahuni akiwa kuhani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Bwana wetu ambaye mambo hayo yote yanasemwa juu yake, alikuwa wa kabila lingine, na wala hakuna hata mmoja wa kabila lake aliyepata kutumikia madhabahuni akiwa kuhani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye ambaye ndiye anayesemwa katika mambo haya, alikuwa wa kabila jingine na hakuna mtu wa kabila hilo aliyekuwa amehudumu katika madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye ambaye mambo haya yanasemwa alikuwa wa kabila lingine, na hakuna mtu wa kabila hilo aliyewahi kuhudumu katika madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kabila nyingine, ambayo hapana mtu wa kabila hilo aliyeihudumia madhabahu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Bwana wetu ambaye mambo hayo yote yanasemwa juu yake, alikuwa wa kabila lingine, na wala hakuna hata mmoja wa kabila lake aliyepata kutumikia madhabahuni akiwa kuhani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani yule aliyesemwa yale maneno alikuwa wa shina jingine, ambalo hakutoka kwake mtu ye yote aliyefanya kazi ya utambikaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kabila nyingine, ambayo hapana mtu wa kabila hiyo aliyeihudumia madhabahu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Bwana wetu ambaye maneno haya yanamwelekea, alikuwa mutu wa kabila lingine, wala hakuna hata mutu mumoja wa kabila lake aliyefanya kazi ya ukuhani kwenye mazabahu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kahila nyingine, wala hapana mtu wa kahila hii aliyeikhudumia madhbahu.