Hebrews 7:14 — Compare Translations
13 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Inafahamika wazi kwamba yeye alizaliwa katika kabila la Yuda ambalo Mose hakulitaja alipokuwa anasema juu ya makuhani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda, tena kuhusu kabila hilo Musa hakusema lolote kwa habari za makuhani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lo lote juu yake katika mambo ya ukuhani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Inafahamika wazi kwamba yeye alizaliwa katika kabila la Yuda ambalo Mose hakulitaja alipokuwa anasema juu ya makuhani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Inafahamika wazi kwamba yeye alizaliwa katika kabila la Yuda ambalo Mose hakulitaja alipokuwa anasema juu ya makuhani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda, tena kuhusu kabila hilo Mose hakusema lo lote kwa habari za ukuhani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana ni dhahiri kwamba Isa Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda, tena kuhusu kabila hilo Musa hakusema lolote kwa habari za makuhani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambalo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Inafahamika wazi kwamba yeye alizaliwa katika kabila la Yuda ambalo Mose hakulitaja alipokuwa anasema juu ya makuhani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hujulikana: Bwana wetu alitoka katika shina la Yuda, nalo shina hilo Mose hakuliambia hata neno moja la utambikaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lo lote juu yake katika mambo ya ukuhani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana inajulikana wazi kwamba Bwana wetu alitoka katika kabila la Yuda, na juu ya kabila lile Musa hakusema hata neno moja linaloelekea ukuhani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote la kuikhusu katika mambo ya ukuhani.