Hebrews 7:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye hakufanywa kuhani kwa sheria na maagizo ya kibinadamu, bali kwa nguvu ya uhai ambao hauna mwisho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
yeye ambaye amefanyika kuhani si kwa misingi ya sheria kama ilivyokuwa kwa baba zake, bali kwa misingi ya uwezo wa uzima usioharibika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alifanywa kuhani, lakini siyo kwa sababu alikamilisha mahitaji ya kuzaliwa katika familia sahihi. Alifanyika kuhani kwa nguvu ya uhai ambayo haitakwisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye hakufanywa kuwa kuhani kwa sheria na maagizo ya kibinadamu, bali kwa nguvu ya uhai ambao hauna mwisho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye hakufanywa kuhani kwa sheria na maagizo ya kibinadamu, bali kwa nguvu ya uhai ambao hauna mwisho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
yeye ambaye amefanyika kuhani si kwa misingi ya sheria kama ilivyokuwa kwa baba zake, bali kwa misingi ya uwezo wa uzima usioharibika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
yeye ambaye amefanyika kuhani si kwa misingi ya sheria kama ilivyokuwa kwa baba zake, bali kwa misingi ya uwezo wa uzima usioharibika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na kikomo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye hakufanywa kuhani kwa sheria na maagizo ya kibinadamu, bali kwa nguvu ya uhai ambao hauna mwisho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
yeye utambikaji wake haukutoka kwenye Maonyo yaagizayo mambo ya kimtu, ila umetoka kwenye nguvu ya uzima usiolegezeka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyu mwingine hakuwekwa kuwa kuhani kwa amri ya kimutu kufuatana na ukoo wake, lakini kufuatana na uwezo wa uzima usiokuwa na mwisho.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
asiyekuwa kuhani kwa sharia ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na kikomo: