Hebrews 7:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
naye Abrahamu akampa sehemu moja ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo. (Maana ya kwanza ya jina Melkisedeki ni “Mfalme wa Uadilifu;” na, kwa vile yeye alikuwa mfalme wa Salemu, jina lake pia lina maana ya “Mfalme wa Amani.”)
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye Ibrahimu alimpa sehemu ya kumi ya kila kitu. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake ni “mfalme wa haki”. Na pia “mfalme wa Salemu” maana yake ni “mfalme wa amani”.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Ibrahimu akampa sehemu ya kumi ya kila kitu alichokuwa nacho. Jina Melkizedeki, mfalme wa Salemu, lilikuwa na maana mbili. Kwanza, Melkizedeki inamaanisha “mfalme wa haki.” Na “mfalme wa Salemu” inamaanisha “mfalme wa amani.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
naye Abrahamu akampa sehemu ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo. (Maana ya kwanza ya jina hili Melkisedeki ni “Mfalme wa Uadilifu”; na, kwa vile yeye alikuwa mfalme wa Salemu, jina lake pia lina maana ya “Mfalme wa Amani.”)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
naye Abrahamu akampa sehemu moja ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo. (Maana ya kwanza ya jina Melkisedeki ni “Mfalme wa Uadilifu”; na, kwa vile yeye alikuwa mfalme wa Salemu, jina lake pia lina maana ya “Mfalme wa Amani.”)
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ambaye Abrahamu alimpa sehemu ya kumi ya kila kitu. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake “mfalme wa haki”; pia “mfalme wa Salemu,” maana yake “mfalme wa amani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye Ibrahimu alimpa sehemu ya kumi ya kila kitu. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake ni “mfalme wa haki.” Na pia “mfalme wa Salemu” maana yake ni “mfalme wa amani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambaye Abrahamu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
naye Abrahamu akampa sehemu moja ya kumi ya vitu vyote alivyokuwa navyo. (Maana ya kwanza ya jina Melkisedeki ni “Mfalme wa Uadilifu;” na, kwa vile yeye alikuwa mfalme wa Salemu, jina lake pia lina maana ya “Mfalme wa Amani.”)
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Aburahamu akamgawia fungu la kumi la mali zote. Maana ya jina lake kwanza ni kwamba: Mfalme wa wongofu; tena ni kwamba: Mfalme wa Salemu, ndio mfalme wa utengemano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
naye Abrahamu akamupa fungu moja la kumi la vitu vyote alivyoteka. Maana ya jina la Melkisedeki, kwanza ni “Mufalme wa haki,” tena ni mufalme wa Salemu, ni kusema “Mufalme wa amani.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
aliyegawiwa na Ibrahimu sehemu ya kumi ya vitu vyote; (kwanza kwa tafsiri, mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemi, maana yake, mfalme wa amani;